Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na Waziri wa Uchina wajadili hali kwenye rasi ya Korea

Ban na Waziri wa Uchina wajadili hali kwenye rasi ya Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, hii leo amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Uchina, Bw. Wang Yi, na kumpa risala ya hongera kwa kuteuliwa kwake hivi karibuni.

Katika mazungumzo hayo, Bwana Ban na Bwana Wang wamejadilina kuhusu matukio ya hivi karibuni kwenye rasi ya Korea, na kuelezea wasiwasi wao kuhusu hali inayozidi kuwa tete katika eneo hilo.

Bwana Ban ameahidi kuafanya lolote awezavyo ili kuifanya hali hiyo tete kuondolewa, akiongeza kuwa ana matumaini makubwa kuwa uongozi wa Uchina utafanya kila uwezalo pia kuifanya hali kutengamaa, na kuisaidia serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa Korea, DPRK, kubadili mkondo wake.