Suala la ubakaji makambini Somalia lamulikwa na UM

6 Aprili 2013

Takriban mwezi mmoja tangu mkutano uliojadili  hadhi ya wanawake ufanyike mjini New York sanjari na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyojikita katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi kwenye maeneo ya vita Bi Hawa Bangura amejikita katika mapambano hayo.

Ziara hii inakuja wakati huu ambapo ripoti ya kutetea haki za binadamu Human Rights Watch inasema kuwa makundi yaliyojihami yakiwemo majeshi mbalimbali yamefanya vitendo vya ubakaji kwa wakimbizi nchini Somalia.

Ripoti hiyo imewanukuu wanawake waliodai kubakwa makambini huku pia wanawake hao wakitaja hofu ya kutengwa na jamii na kukumbana na unyanyapaa wanaporipoti kuwa wamebakwa.

Ungana na Joseph Msami basi, katika kuangazia safari ya Bi Bangura nchini Somalia ambayo huenda ikaleta tumaini jipya kwa waathirika na mapambano dhidi ya ukatili wa kimapenzi kwa ujumla.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter