Umoja wa Mataifa waongoza kampeni ya kupima shinikizo la damu

7 Aprili 2013

Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza shinikizo la damu kuwa zingatio kuu wakati huu dunia ikiadhimisah Siku ya Afya Duniani.

Kwa kutambua umuhimu wa hilo, na kama hatua ya kutoa mfano, Umoja wa Mataifa umeandaa zoezi maalum la upimaji wa shinikizo la damu kwa  wafanyakazi wake na watu wengine mjini New York, na kwingineko mashirika yake yanapopatikana, likiwemo Shirika la Afya Duniani.

Mwandishi wetu Joseph Msami amefika katika eneo la tukio na kutuandalia ripoti ifuatayo

(Ripoti ya Joseph Msami)