Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kukumbuka mauaji ya kimbari Rwanda

Umoja wa Mataifa kukumbuka mauaji ya kimbari Rwanda

Leo ni siku ilotengwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kumbulumbu ya mauaji ya kimbari yalotokea miaka 19 iliyopita nchini Rwanda. Watu wapatao laki nane waliuawa nchini Rwanda katika kipindi cha siku mia moja mnamo mwaka 1994 nchini Rwanda.

Katika kuadhimisha siku hii, Umoja wa Mataifa na watu kote duniani hufanya hafla maalum zinazojumuisha kuwasha mishumaa na kuwa kimya kwa dakika moja ili kuwaenzi wahanga wa mauaji hayo. Hapa mjini New York, Umoja wa Mataifa utaikumbuka siku hiyo kwa hafla maalum mnamo tarehe 9 Aprili.

Miongoni mwa wanaoikumbuka siku hii, ni Eugenie Mukeshimana, ambaye babake na mumewe waliuawa katika mauaji hayo, wakati akiwa na mamba ya miezi minane. Eugenie amemwelezea Joshua Mmali kuhusu hisia zake sasa na kile anachofanya kupitia mtandao walioanzisha wa manusura wa mauaji ya kimbari, yaani Genocide Survivors Support Network, wenye makao yake Jimbo la New Jersey, Marekani.

(MAHOJIANO)