Tumejifunza kutoka Rwanda, tunachukua hatua: Ban

6 Aprili 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa salamu kwa kumbukumbu ya miaka 19 tangu mauaji ya kimbari ya Rwanda na kusema yaliyotokea nchini humo ni fundisho na kwamba ofisi yake inachukua hatua kila siku kuhakikisha tukio kamahilohalitokei tena. Bwana Ban amesema mathalani mshauri wake anayehusika na hatua za kuepusha mauaji ya kimbari, anafuatilia viashiria vyovyote vile duniani vinavyoweza kuwa chanzo cha tukio la namna hiyo.  Amesema wajibu wa kulinda binadamu kwa sasa umekuwa ndio kanuni ya kimataifa na kwamba pamoja na hatua hizo, Umoja wa Mataifa unahakikisha wale wote wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kimbari hawakwepi mkono wa sheria. Halikadhalika Katibu Mkuu amesifuRwandakwa mwelekeo mpya baada ya tukio la mwaka 1994 na kusihi serikali na wananchi wake kuendeleza moyo wa utengamano, maridhiano na ujenzi wa taifa