Msaada wa UNICEF kwa wakimbizi wa Syria Jordan uko njia panda:

5 Aprili 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema huenda likalazimika kusitisha ugawaji wa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 wa Syria walioko Jordan kutokana na ukosefu wa fedha.

UNICEF inasema ifikapo Juni mwaka huu halitokuwa na uwezo wa kutoa huduma za maji salama, usafi, chanjo, elilmu na ulinzi kwa wakimbizi wa Syria walioko katika kambi ya Za'atari nchini Jordan.

Hadi sasa wafadhili wamechangia dola milioni 12 kwa UNICEF wakati ombi lililotolwa kwa operesheni zake Jordan ni dola milioni 57.

Marixie Mercado wa UNICEF anasema mahitaji ya wakimbizi yanaongeza kwa kasi kubwa na kupita kiasi cha rasilmali zilizopo kwa sasa.

"Mahitaji yanaongezeka haraka na hatuna fedha zozote. Hii ina maana kwamba ifikapo mwezi Juni tutasita kupeleka lita milioni 3.5 za maji kila siku katika kambi ya Za'atari. Ni kusema hatutoweza kufungua shule ya tatu ambayo tunajenga katika kambi hiyo kutokana na ukosefu hatuna fedha za kulipia mishahara ya walimu, kununua vitabu, samari na gharama za kuendesha shule. Hii inamaana kuwa Wizara ya Elimu itawafukuza wanafunzi wakimbizi wa Syria wanaojaribu kuingia shule za Jordan kwa sababu hatataweza kusaidia watoto wa shule kutoka Syria zaidi ya wale 30,000 tunaosaidia tayari katika shule za Jordan.