Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanza kuhesabu siku 1000 hadi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia

UM waanza kuhesabu siku 1000 hadi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia

Umoja wa Mataifa umeanza leo kuhesabu siku elfu moja hadi kufikia tarehe ya mwisho ya kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia. Katika ujumbe wake wa awali, Katibu Mkuu Ban Ki-moon, amesema juhudi zaidi zinatakiwa ili kutimiza malengo yalosalia, akisisitiza kuwa njaa na utapiamlo vinaweza kutokomezwa.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa idadi ya watu, UNFPA Babatunde Osotimehin amesema, inagwa kuna hatua kubwa za ufanisi zilizopigwa, malengo ya milenia nambari 5 (a) na (b) kuhusu afya ya mama na uzazi ndiyo yaliyosalia nyuma zaidi.

(SAUTI BABATUNDE)