Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasikitishwa na vurugu zilizotokea kwenye kituo kimoja Indonesia

UNHCR yasikitishwa na vurugu zilizotokea kwenye kituo kimoja Indonesia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa limevunjwa moyo na kusikitishwa kufuatia taarifa za kuzuka kwa hali ya sintofahamu kwenye kituo cha Medan kilichoko Kaskazini mwa jimbo la Sumatra nchini Indonesia.

Duru za habari zinasema kuwa, kituo hicho kilikumbwa na machafuko yaliyohusisha waomba hifadhi na jamii ya watu wa Myanmar. Watu nane walipoteza maisha huku wengine 15 wakijeruhiwa.

UNHCR imetaka kuwepo kwa hali ya utulivu na imeitaka serikali ya Indonesia kuchukua hatua za kuzuia kutojirudia tena kwa hali kama hiyo.