Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasikitishwa na ongezeko la adhabu ya kifo

UM wasikitishwa na ongezeko la adhabu ya kifo

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imesema nchi nyingi za Mashariki ya Kati na bara la Asia zimepuuza wito wa kusitishwa kwa adhabu ya kifo na kunyonga wahalifu, na zinaendelea kutekeleza adhabu hiyo inayokiuka misingi ya haki za binadamuTaarifa zaidi na Joseph Msami:

TAARIFA YA MSAMI

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu mapema wiki hii watu watatu walinyongwa Kuwait hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwezi Meyi mwaka 2007, wakati nchi ya Iraq inaripotiwa kunyonga watu 12 mwaka huu.

Barani Asia adhabu ya kifo imetekelezwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mingi katika nchi za India na Indonesia, wakati Japan ikirejesha unyongaji mwaka 2012. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, idadi ya watu isiyofahamika wamekuwa wakinyongwa nchini China, Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea na Iran.

Rupert Colville ni afisa kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, na anasema unyongwaji bado unaendelea licha ya ya jumuiya ya kimataifa kupaza sauti ya kukomesha adhabu ya kifo.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)