Kuelekea kikomo cha MDGs Burundi yapiga hatua, elimu

4 Aprili 2013

Ikiwa kikomo cha malengo ya milenia kinakaribia mwaka 2015 nchi mbalimbali zinajitahidi kufikia malengo hayo ambapo  nchini Burundi nchi iliyoko Afrika Mashariki, imepiga hatua katika kuandikisha elimu ya msingi kwa watoto wanaosatahili.

Mathalani takwimu zinonyesha kwamba mwaka 2004 wavulana na wasichana walioandikishwa kuanza elimu ya msingi nchini Burundi ni asilimia 57.

Takwimu za serikali pia zinaonyesha kwamba serikali hiyo iliyoanza mpango wa elimu ya msingi bure kwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka 15 mwaka 2005, imefanikiwa kuwawezesha  wale wasio na uwezo kupeleka watoto wao shule.

Licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika kufikia lengo hilo la pili la mendeleo ya millennia, MDGS hiyo ni hatua inayoonyesha dalili njema tunapoelekea mwajka 2015,ungana na Ramadhani Kibuga katika taarifa ifuatayo.