Uchina yatajwa kuongoza kama chanzo cha watalii kote duniani

4 Aprili 2013

Kwa karne iliyopita Uchina imekuwa  nchii inayowatoa watalii wengi duniani kote kufuatia kuimarika kwa miji, mapato ya juu na kulegezwa kwa masharti ya kusafiri kwenda nchi za kigeni.

Idadi ya wasafiri wa kichina kimataifaa imeimarika kutoka millioni 10 mwaka 2000 hadi milioni 83 mwaka 2012, huku matumizi yao ya fedha katika nchi za kigeni yakiongezeka mara 8 zaidi tangu mwaka 2000.

Kufuatia kuimarika kwa  uchumi, Uchina imekuwa na matumizi ya  juu zaidi katika utalii wa kigeni mwaka 2012 na kuzipeku nchi zenye utalii mwingi zaidi zamani, kama Ujerumani ambayo ilikuwa ya kwanza,  na Marekani ambayo zamani ikichukua nafasi ya pili.

Katibu Mkuu wa Shirika la UM maswala ya Utalii UNWTO, Taleb Rifai, amesema bado mataifa ya chumi zinazoendelea yanaendelea  kuimarika katika mahitaji ya utalii , na kuongeza kuwa kuimarika kwa matumizi ya utalii kwa Uchina na Urusi kunadhihirisha kuingia katika soko la utalii kwa nchi za mapato wastani, jambo ambalo litabadili sura ya utalii duniani.