Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bangura akutana na viongozi wa Kenya na wahanga wa ukatili wa kimapenzi:

Bangura akutana na viongozi wa Kenya na wahanga wa ukatili wa kimapenzi:

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi kwenye maeneo ya vita Bi Hawa Bangura leo yuko Nairobi Kenya ambako amekuwa na mkutano na viongozi wa Kenya na vyombo vya habari. Joshua mmali na taarifa kamili.

(SAUTI YA JOSHUA MMALI)

Akizungumza mjini Nairobi Bi. Bangura  amesema ili kutokomeza ukatili wa kimapenzi ofisi yake imeweka mikakati sita ambayo ni kutowafumbia macho wanaoendesha vitendo hivyo na kuhakikisha haki kwa wahanga, pili kuwalinda na kuwawezesha raia wanaokabiliwa na ukatili wa kimapenzi hasa wanwake na wasichana, kushawishi viongozi wa kisiasa kulivalia njuga suala hili, kuimarisha ushirikiano baina ya serikali na mfumo wa Umoja wa mataifa, kutambua kuwa ubakaji unatumika kama mbinu za vita na mwisho kusistiza uwajibikaji katika vita dhidi ya ukatili huo.