Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitisho vya Korea ya Kaskazini vyamtia hofu Ban Ki-moon

Vitisho vya Korea ya Kaskazini vyamtia hofu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema anatiwa hofu na kusumbuliwa na ongezeko la vitisho na mvutano kwenye ghuba ya Korea na hasa vitisho vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK.

Amelitaka taifa hilo kuzingatia maazimio ya baraza la usalama, na kuongeza kuwa baraza hilo limepitisha maazimio matatu ya vikwazo dhidi ya DPRK ikiwemo vya kufanya majaribio ya silaha na kurusha makombora.

Ameitaka DPRK kutekeleza maazimio hayo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)