Madhara ya mabomu ya kutegwa ardhini ni dhahiri: Ban

4 Aprili 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake wa siku ya ya kuhamasisha na utoaji msaada wa kutokomeza matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini hii leo na kupaza sauti juu ya athari za silaha hizo kwenye maeneo ya migogoro kama vile Mali na Syria.

Ametaja madhara hayo kuwa ni yale ya kibinadamu na kwamba Umoja wa Mataifa unasaidia kubaini na kutegua mabomu hayo. Hata hivyo amesema jitihada zaidi zahitajika ikiwemo nchi zote wanachama kutia saini na kuridhia mikataba kama ule wa mwaka 1997 wa kupiga marufuku matumizi ya mabomu hayo kwa lengo la kuimarisha amani duniani na kutoa fursa ya maendeleo.

Laos ni miongoni mwa nchi zinazosaidiwa na Umoja wa Mataifa kutegua mabomu hayo, na baada ya vita vilivyomalizika miaka 30 iliyopita, madhara ya matumizi ya mabomu hayo ni dhahiri.

Balozi Saleumxay Kommasith [Salem-psy Komasith] ni mwakilishi wa kudumu wa Laos katika Umoja wa Mataifa.

(Sauti Balozi)