WFP imeanza kuwalisha watoto wakimbizi wa Syria walioko Jordan na Iraq

4 Aprili 2013

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limezindua mradi wa kuwalisha watoto mashuleni. Watoto zaidi ya 10,500 ambao ni Wasyiria wanaohudhuria masomo kwenye kambi za wakimbizi za Jordan na Iraq watafaidika na mpango huo wenye lengo la kuboresha lishe na kuhamasisha watoto kuhudhuiria shule.

Jordan watoto zaidi ya 6000 wanapokea chakula cha mchana katika shule mbili zinazoendeshwa na UNICEF kwenye kambi ya Zaatari, huku wenginge zaidi ya 4500 wakipokea chakula kwenye kambi ya Domiz eneo la Dohuk Kaskazini mwa Iraq na kwenye kambi zingine mbili mjini Al-Qaim Katikati mwa Iraq.

Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)