Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili Mali na ulinzi wa amani

Baraza la Usalama lajadili Mali na ulinzi wa amani

Mashauriano ya leo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusuMaliyamezingatia ripoti ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon iliyowasilishwa na Mkuu wa masuala ya siasa ndani ya Umoja huo Jeffrey Feltman. Ripoti hiyo pamoja na kuelezea hali halisi ya usalama na kibinadamu kuwa bado ni mbaya inapendekeza hatua za kuchukuliwa ili mafanikio ya kiusalama yaliyopatikana yaweze kulindwa. Mathalani, Feltman amesema pamoja na kuanzishwa kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchiniMali, UNOM, kuna umuhimu wa kutofautisha majukumu ya ulinzi wa amani.  Amesema bila kufanya hivyo Umoja wa Mataifa hautaweza kuweka mfumo wake wa kina na mpana unaohitajika kushughulikia vyanzo thabiti vya mizozo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambavyo vinatoa taswira pana ya mgogoro wa Mali.

 (SAUTI – FELTMAN)

 “Katibu Mkuu amebaini kuwa itakuwa muhimu kutofautisha kati ya majukumu ya msingi ya ulinzi wa amani ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu na shughuli za kuimarisha amani na kudhibiti ugaidi za jeshi litakalokuwepo..Bila kuweka bayana tofauti ya majukumu haya,  wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wa kusambaza misaada na wale wanaofuatilia usimamizi wa haki za binadamu watashindwa kufanya kazi zao katika mazingira salama.