Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pima shinikizo la damu yako, punguza hatari: WHO

Pima shinikizo la damu yako, punguza hatari: WHO

Takriban watu bilioni moja kote duniani wanakadiriwa kuathiriwa na shinikizo la damu, hali ambayo inaathiri kila mtu mmoja kati ya watatu wenye umri wa zaidi ya miaka 25.

Idadi kubwa zaidi ya watu walioathirika na shinikizo la damu wapo barani Afrika, linakoathiri asilimia 46 ya watu wazima.

Kwa mujibu wa WHO, shinikizo la damu ni moja ya vitu vinavyochangia zaidi ugonjwa wa moyo na kiharusi, ambavyo kwa pamoja huchangia kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya mapema na ulemavu. Shinikizo la damu pia huongeza hatari ya kuharibika figo na upofu.

Kabla ya Siku ya Afya Duniani, Aprili Saba, WHO imewataka watu wapime  na kuzuia au kudhibiti shinikizo la damu. Daktari Shanthi Mendis ni mtaalamu wa WHO.

(SAUTI Dr. Mendis )

“Mara nyingi hakuna dalili, hadi unapopata matatizo. Watu wanatakiwa wajue vipimo vyao. Kupunguza ulaji wa chumvi katika vyakula, kula matunda na mboga, kupunguza matumizi hatari ya pombe, kufanya mazoezi ya kudhibiti uzito na kuhakikisha huli chakula kingi na kuongeza uzito- vyote hivi vinachangia kuzuia shinikizo la damu”