Mamilioni wameathirika na ugonjwa wa mtindio wa ubongo

2 Aprili 2013

Ugonjwa wa mtindio wa ubongo unaoathiri ukuaji wa mwili umemulikwa hii leo ambayo ni siku ya kuhamasisha dunia juu ya ugonjwa huo ambao umeenea maeneo yote duniani.

Shirika la afya duniani, WHO linaeleza kuwa ugonjwa huo hujitokeza mwanzoni kabisa mwa uhai wa mwanadamu na chanzo ni hitilafu za mishipa ya fahamu ambayo hatimaye huathiri utendaji wa ubongo.

Balozi Abulkalam Abdul Momen wa Bangladesh amesema  kati ya watoto 88 duniani wanaokumbwa na ugonjwa huo, 54 ni wavulana.

(SAUTI ya Balozi Abulkalam)

Hata hivyo katika ujumbe wake kwa siku ya leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema tafiti zinadhihirisha kuwa tiba ya mapema dhidi ya ugonjwa huo inaweza kusaidia mgonjwa kuimarika na kupata nafuu zaidi.

Akizungumzia siku hiyo Ban Soon-taek ambaye ni mke wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, ametaka jumuiya ya kimataifa kumulikia zaidi ugonjwa huo ili kuboresha maisha ya mamilioni ya watu wanaoishi na mtindio wa ubongo.

(SAUTI – Bi. Ban Soon-Taek)