Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yazidi kuwa tete kwa wahamiaji nchini Yemen, IOM yarejelea ombi la msaada

Hali yazidi kuwa tete kwa wahamiaji nchini Yemen, IOM yarejelea ombi la msaada

NchiniYemen, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM linaendelea kutoa ombi la kupata dola Milioni Tano kwa ajili ya kusaidia wakimbizi waEthiopianaSomaliawaliokwama nchini humo baada ya kushindwa kuendelea na safari zao za ughaibuni. Mazingira ya kibinadamu ni magumu, wengine wanafariki dunia na wengine hususan wanawake na watoto wako hatarini kukumbwa na ukatili. Uhasama umeshamiri baina ya wenyeji na wahamiaji. Jumbe Omari Jumbe, msemaji wa IOM aliulizwa na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali halisi ya kibinadamu na hatma ya usaidizi.

 (Mahojiano)