Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 AMISOM yatoa mafunzo ya kijeshi Somalia

 AMISOM yatoa mafunzo ya kijeshi Somalia

Vikosi vya muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM vimekuwa vikitoa misaada kadhaa ya kijeshi ikiwemo kusaidia katika ulinzi na usalama wa nchi hiyo ambayo imeshuhudia mizozo kwa miongo kadhaa.

Misaada ya AMISOM imekwenda mbali  ambapo sasa wanatoa mafunzo ya kijeshi kwa majeshi ya nchi hiyo.

Hivi karibuni Umoja wa Ulaya ulitoa msaada wa euro milioni 33 kwa vikosi hivyo ili kusaidia kuimarisha na kujenga upya serikali ya Somalia.

Ungana na Joseph Msami katika taarifa inayoangazia namna AMISOM Imejikita katika kuimarisha usalama nchini Somalia kwa kutoa mafunzo ya kijeshi na  kusaidia kuimarisha utawala wa kisheria.