Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makambi zaidi yanahitajika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Syria: UNHCR

Makambi zaidi yanahitajika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Syria: UNHCR

Misongamano kwenye kambi waliko wakimbizi kutoka Syria imekuwa ni tatizo kubwa katika utoaji wa misaada kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kwa sasa UNHCR inatoa wito kwa serikali katika eneo hilo kutoa nafasi kwa ujenzi wa kambi zaidi.

Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa huduma za usafi zimekuwa zikidorora chini ya viwango vya kimataifa kutokana na kuwepo kwa misongamano huku hali ya joto ikichangia kuwepo kwa mikurupuko ya magonjwa na kuwepo kwa misukosuko kwenye kambi.

(SAUTI YA ADRIAN)