Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimaye Baraza Kuu lapitisha mkataba wa kudhibiti biashara ya silaha duniani

Hatimaye Baraza Kuu lapitisha mkataba wa kudhibiti biashara ya silaha duniani

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha nyaraka ya mwisho ya Mkataba wa kimataifa wa kudhibiti biashara ya silaha duniani, ATT ambayo ilishindwa kupitishwa katika mkutano wa mwisho wa mkataba huo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rais wa Baraza hilo Vuk Jeremic amewaambia wajumbe kuwa kupitishwa kwa mkataba huo ni jambo muhimu katika kuepusha matumizi ya silaha yanayozua mizozo na kuweka amani ya kudumu duniani.

(SAUTI YA VUK JEREMIC)