Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka DPRK kumaliza mvutano wa nyuklia

Ban aitaka DPRK kumaliza mvutano wa nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumzia mvutano wa nyukilia katika rasi ya Korea na kusema amesikitishwa na kukua kwa mgogoro huo ambao ameuita usio wa lazima kwa kuwa anaamini hakuna mtu mwenye lengo la kuishambuilia rasi hiyo kutokana na tofauti za mfumo wa siasa na sera za nje.

Bwana Ban amewaambia waandishi wa habari nchini Andorra kwamba yuko tayari kusaidia katika kutatua mvutano huo na kutoa mwito wa kumaliza mvutano ambao amesema matokeo yake ni kuzorotesha amani.

(SAUTI YA BAN)