Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maiti za wahamiaji waliokwama Yemen kuzikwa mjini Haradh: IOM

Maiti za wahamiaji waliokwama Yemen kuzikwa mjini Haradh: IOM

Hatimaye halmashauri ya mji wa Haradh ulioko Kaskazini mwa Yemen imeridhia kuzika maiti Ishirini na watano ya wahamiaji waliokuwa wamerundikwa katika chumba kimoja mjini humo karibu na ofisi za shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM. Hatua hiyo imekuja tarkibani wiki moja baada ya IOM kuripoti taarifa hizo wakati huu ambapo shirikahilolinakabiliwa na ukata na halijaweza kupata dola Milioni Tano za dharura kutoa misaada ya kibinadamu pamoja na kuwarejesha makwao wahamiaji waEthiopianaSomaliawaliokwama nchini Yemeni. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM na amefafanua zaidi.

 (SAUTI YA JUMBE)