UNESCO na washirika kukuza matumizi ya kemia.

1 Aprili 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni , UNESCO, kampuni moja ya nchini Urusi PhosAgro na taasisi ya kemia IUPAC zimetia saini makubaliano ya kushirikiana katika mradi wa kuendeleza wanasayansi chipukizi wanaofanya utafiti mbalimbali kwa kutumia teknologia ya kemia katika nchi zinazoendelea.

Mradi huo unaoelenga kuchochea matumizi ya kemia yanayohifadhi na kulinda mazingira utatiwa shime kwa dola za kimarekani milioni moja nukta nne kama kiwango cha kuanzia umetiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova na Mtendaji Mkuu wa PhosAgro Maxim Volkov ambapo wote wameelezea jinsi mradi huo utakavyonufaisha wanasayansi hao.

Mkuu wa UNESCO amesema mradi huo utasaidia nchi nyingi zinazoendela ambazo zimekuwa na uhitaji mkubwa wa kuendekeza uwezo wa tafiti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira na teknologia ya sauti ya mazingira huku mkuu wa kampuni ya PhosAgro akisema mradi huo ni uwekezaji kwa sayari yote ya dunia na mfano mzuri wa namna sayansi na biashara zinavyoweza kuungana chini ya mwavuli wa UNESCO kujenga uelewa mpya kuhusu kulinda mazingira.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mradi huo, kipaumbele kitakuwa katika kulinda mazingira, afya, mgawanyo wa chakula pamoja na rasilimali asilia na mada za tafiti zitachaguliwa na kusimamiwa na jopo la wataalamu wa kimataifa.

Akizungumzia hatua hiyo Derrick Harvey ambaye ni mtaalamu wa Unesco wa  radio za kijamii jijini nchini Tanzania amesema changamoto kubwa ni kuzifikisha hela hizo kwa walengwa na kuahidi kutimiza wajibu huo kwa kupitia redio za kijamii nchini Tanzania.

(SAUTI YA Derrick Harvey)