Ban azungumza kwa simu na Uhuru na Odinga

1 Aprili 2013

Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidiaKenya,  na kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon baada ya Mahakama Kuu nchini humo kutoa uamuzi wa pingamizi la uchaguzi mkuu uliobainisha kuwa ulikuwa huru na wa haki.

Bwana Ban alitoa ujumbe huo alipoongea kwa njia ya simu na Uhuru Kenyatta akimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya huku akiongea pia na waziri Mkuu Raila Odinga akimpongeza kwa kukubali uamuzi wa mahakama huku akiwataka wakenya kuendelea na mazingira ya amani na utulivu.

Uhuru akizungumza baada ya uamuzi wa Mahakama alishukuru pande zote na kusema kuwa serikali yake itakuwa jumuishi ili kuakisi hali halisi yaKenya.

(SAUTI YA UHURU)

Naye Waziri Mkuu Odinga akasema wamekubali uamuzi na wanaamini katika katiba.

(SAUTI ODINGA)