Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wawaenzi waathiriwa wa Utumwa kwa tamasha la muziki

Umoja wa Mataifa wawaenzi waathiriwa wa Utumwa kwa tamasha la muziki

Tarehe Ishirini na tano Machi ni Siku ya Kuadhimisha Utumwa na Biashara ya Utumwa ya Atlantiki.

Na mapema wiki hii Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilifanya hafla maalum ya kuwakumbuka na kuwaenzi waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa.

Miongoni mwa mfululizo wa matukio ya kumbukumbu hiyo, liliandaliwa tamasha la muziki kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lililowahusisha wanamuziki kutoka barani Afrika na katika maeneo mengine. Kwa mengi zaidi kuhusu tamasha hilo na siku hiyo, ungana na Joshua Mmali katika makala hii…