Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makambi ya wakimbizi wa ndani yalindwe zaidi:UM

Makambi ya wakimbizi wa ndani yalindwe zaidi:UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kulinda makambi ya wakimbizi wa ndani kufuatia shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Pakistan.

Mtaalamu Chaloka Beyani ambaye ni mwakilishi maalumu wa haki za binadamu kwenye makambi ya wakimbizi wa ndani amelaani vikali tukio hilo la Machi 21 kwenye kambi ya Jalozai Kaskazini Magharibi mwa Pakistan na kukatili maisha ya wtu 10 na mnyakazi mmoja wa misaada huku likijeruhi wengine wengi.

Bwana Beyani ameitaka serikali ya Pakistan kuimarisha hatua za usalama na kuboresha mikakati ya ulinzi kuzunguka kambi ya Jalozai pia kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa shambulio hilo.