Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF wawaandalia watoto wakimbizi mazingira rafiki

UNICEF wawaandalia watoto wakimbizi mazingira rafiki

Zaidi ya wakimbizi elfu 68 kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia Rwanda kutafuta makazi kufuatia mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo,  iliyotawaliwa na vita kwa miongo kadhaa.

Utengano wa kifamilia imekuwa ni moja ya kadhia kubwa wanyokutana nayo wakimbizi ambao mara nyingi husambaratika wakati wa kukimbia mapigano. Waathirika wakubwa katika hili ni watoto ambao bado wanahitaji kucheza na kujisikia kama watoto wengine.

 Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia watoto UNICEF limeelekeza nguvu zake kwa watoto ili kuhakikisha wanawapatia nafasi ya kuufurahia utoto wakiwa katika kituo cha wakimbizi cha Nakamira kilichoko nchini Rwanda, nchi ambayo kwa mujibuwa wa takwimu za UNICEF asilimi 65 ya watoto walikabiliwa na ukatili wa kijinsia  mwaka 2011 hiyo ikiwa ni kwa mji mkuu,Kigali pekee.

 Lakini lipo tumaini jipya kwa watoto wakimbizi wanaoshi nchini humo wakitokea Jamhuri ya Kiemkrasi ya Kongo DRC. Ungana na Joseph Msami kufahamu kwa undani.