UNICEF yasaidia watoto wakimbizi Rwanda

28 Machi 2013

Kufuatia maelfu ya wakimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kukimbia na kutafuta hifadhi katika nchi mbalimbali ikiwamo Rwanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia watoto UNICEF, na washirika linahudumia watoto walioko katika kambi hizo ili kuwaandalia mazingira rafiki.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa UNICEF nchini Rwanda Noala Skinner, idadi ya watoto katika kituo cha Nkamira Kaskazini Magharibi mwa wilaya ya Rubavu ni asilimia sitini ya wakimbizi na shirika hilo linawasaidia watoto hao ambao wengi wao wametengana na familia zao.

SAUTI (NOALA SKINNER)

Kwa upande wake mmoja wa watoto katika kituo hicho Yvette Gateyeneza anaeleza namna walivyowezeshwa kujisikia kama watoto wengine.

(SAUTI MTOTO YVETTE GATEYENEZA)

Zaidi ya wakimbizi elfu 68 kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia Rwanda kutafuta makazi kufuatia mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter