Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro wa kibinadamu waongezeka CAR: OCHA

Mgogoro wa kibinadamu waongezeka CAR: OCHA

Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema mgogoro nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwemo kutwaliwa madaraka kwa nguvu kulikofanywa na kundi la Seleka Machi 24 kumechangia hali ya kibainadamu ambayo tayari ni mbaya kuwa mbaya zaidi.

Tangu Desemba mwaka jana inakadiriwa kuwa watu 173,000 wamekuwa wakimbizi wa ndani huku wengine 32,000 wamekimbilia nchi jirani za Jamuhurui ya Kidemokrasia yaCongo,CameroonnaChad.

OCHA inasema shule, benki, maduka makubwa ya bidhaa yamefungwa ambapo msemaji wa ofisi hiyo Amy Martin anaeleza kuwa hali itakuwa ngumu zaidi miezi michache ijayo kwa wakazi Elfu 80 wa maeneo ya kati na kaskazini mwaMali.

(SAUTI YA AMY MARTIN)

Na kwa maelezo zaidi huyu hapa Jason Nyakundi

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)