Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wakutana UM kujadili teknolojia katika maendeleo endelevu

Vijana wakutana UM kujadili teknolojia katika maendeleo endelevu

Ni vipi vijana wanaweza kushiriki kuziba pengo la kidijitali na kuchangia juhudi za kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu, yaani SDGs?

Hilo ndilo lililokuwa swali vichwani mwa mamia ya vijana kutoka kote duniani, wakati wa kongamano ambalo limehitimishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Jumatano jioni.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja vijana wanaojihusisha na mambo ya ubunifu wa kiteknolojia, ili kujadili kuhusu siku zijazo wanazozitaka vijana.

Mmoja wa wahusika walolihutubia kongamano hilo, ni Philip Thigo kutoka Kenya, ambaye ameielezea Redio ya UM ni nini vijana wanachotaka wafanyiwe, na jinsi wanavyoweza kuchangia maendeleo endelevu.

(SAUTI YA THIGO) 36”