Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama latilia shaka usalama wa Milima ya Golan

Baraza la Usalama latilia shaka usalama wa Milima ya Golan

Baraza la Usalama limetaka pande zinazozozana nchini Syria kutohatarisha usalama wa watumishi wa Umoja wa Mataifa walioko katika milima ya Golani.

Katika taarifa yake, Baraza hilo limeelezea masikitiko yake kutokana na kuzidi kuongezeka kiwango cha askari katika eneo hilo ambalo wako watumishi wa Umoja wa Mataifa walioko kwenye kikosi maalumu cha ufuatiliaji zoezi la kuondoa silaha UNDOF.

Kikosi hicho kipo kwenye milima hiyo tangu mwaka 1974 baada ya kuwepo makubaliano ya usitishwaji wa mapigano baina ya Israel na Syria.

Baraza hilo pia limeelezea wasiwasi wake likisema kuwa baadhi ya wakazi kwenye maeneo hayo wanakumbwa na vitisho vya usalama.