Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano huko Jonglei yasababisha watu kukimbilia Kenya umesema UM

Mapigano huko Jonglei yasababisha watu kukimbilia Kenya umesema UM

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu imesema mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali ya Sudan Kusini na vikundi vyenye silaha huko Jonglei yamezidi kuathiri maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari kuwa kuzorota kwa usalama hususan kwenye maeneo ya barabarani kunakwamisha operesheni za kusambaza misaada muhimu.

Hata hivyo amesema licha ya hali hiyo wafanyakazi wanajitahidi kugawa misaada muhimu ikiwemo vyakula na maji. Imeelezwa kuwa mapigano hayo yamesababisha wakazi wa Jonglei kukimbilia Kenya.

(SAUTI YA MARTIN NERSIKY)