Sellström azungumzia jukumu la kuongoza jopo la uchunguzi Syria

27 Machi 2013

Mkuu wa jopo la Umoja wa Mataifa litakalochunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, Profesa Ǻke Sellström amezungumzia uteuzi huo na kusema ni heshima kubwa kwa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon kumteua kuongoza kikundi hicho.Katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa Sellström amesema kuwa anatarajia kuanza kazi hiyo ndani ya wiki moja au mbili.(SAUTI YA Sellström) 00”30”

“Pengine ndani ya wiki moja au mbili kazi itaanza na nafikiri tuna siku tatu au nne za maandalizi na siku tatu au nne za uchunguzi na wiki mbili au tatu za kuandika ripoti na kufanya uchambuzi wa kemikali.”

Bwana Sellström ni meneja mradi katika taasisi ya utafiti nchini Sweden, ambayo ni kituo cha masomo ya juu kuhusu jamii, usalama na hali za hatari, na hususan matukio makubwa yanayohusisha vitu vya kemikali, bayolojia, na miyale ya nyuklia na vilipuzi.