Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na waziri wa Mambo ya Nje wa DRC

Ban akutana na waziri wa Mambo ya Nje wa DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, Raymond Tshibanda N'Tungamulongo ambapo viongozi hao wamezungumzia hali tete ya usalama nchini humo na utekelezaji wa mkataba wa amani na ushirikaino kwa ajili ya ukanda wa maziwa makuu.

Viongozi hao pia wamekubaliana kwamba maazimio yajayo ya  baraza la usalama la umoja wa mataifa yalenge katika kuimarisha ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini DRC Kongo MONUSCO ili  kutekeleza lengo la Katibu Mkuu la kufahamu kwa kina chanzo cha migogoro katika eneo la nchi za maziwa makuu.

Mapema  Bwana Ban alifanya mazungumzo na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  ya Kongo Joseph Kabila.