Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa huduma kwa waathiriwa wa mvua kubwa

UNHCR yatoa huduma kwa waathiriwa wa mvua kubwa

Shirika la Kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR limekuwa likitoa huduma za hema na viandarua kwa familia zilizoathirika kutokana na mvua kubwa huko Gori na Koptinari. Kufuatia ombi kutoka kwa mamlaka za Georgia, wawakilishi UNHCR nchini Georgia wanawasaidia waathiriwa wa mvua kubwa na kimbunga Gori.

Shirika la UNHCR limetoa hema 100 kwa familia zinazoishi Gori hema na kuwapa vyandarua vya kufunikia paa za nyumba wakaazi wa Kopitnari, eneo la Imereti.

UNHCR inatoa huduma na kulinda takriban watu 280,000 waliohatarini Georgia wakiwemo wakimbizi wa ndani 270,000 na zaidi ya watu 1000 wasio makwao, zaidi ya watu 400 wanaoomba uhamiaji na wakimbizi 300.