UNHCR yasambaza huduma za dharura kuwanusuru wakimbizi walionusurika na moto Thailand

26 Machi 2013

Wakati idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Thailand ikiongezeka na kutokana na kuzuka kwa moto kwenye kambi moja ya wakimbizi, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi hao UNHCR limeanza kusambaza misaada ya dharura.

Ripoti zinasema kuwa, moto uliozuka kwenye kambi ya Ban Mae Surin iliyoko katika jimbo la Mae Hong imeteketeza kambi hiyo na hadi sasa wakimbizi waliopoteza maisha wamefikia 37.

Maelfu wengine ya raia kwenye eneo hilo wamekosa makazi baada ya nyumba zao kuungua kwa moto.Pia kumeshudiwa uharibu mkubwa ikiwemo kuungua kwa baaadhi ya shule na sehemu za huduma muhimu.

Serikali ya Thailand imehaidi kuanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo na tayari UNHCR imeanza kusambaza huduma za dharura.