Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaomba dola milioni 7.1 kusaidia Guinea Bissau

WFP yaomba dola milioni 7.1 kusaidia Guinea Bissau

Shirika la Mpango wa Chakula, WFP, limesema taifa la Guinea Bissau linahitaji kwa dhrura ufadhili wa dola milioni 7.1 zitakazotumika kuwapa msaada wa chakula na lishe watu 278, 000 kote nchini mwaka 2013.

Usaidizi huu ulitarajiwa kung’oa nanga mwezi Machi mwaka huu lakini unaonekana kuchelewa. WFP haijapokea msaada wowote kwa ajili ya operesheni hiyo.