Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yahaha kukwamua wahamiaji kutoka Ethiopia

IOM yahaha kukwamua wahamiaji kutoka Ethiopia

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM nchini Djibouti  limetoa ombi la dharura la dola Milioni Tano kwa ajili ya kuokoa maisha wahamiaji wa Ethiopia na Somaliawalio kwenye mazingira magumu nchini humo baada ya kushindwa kuendelea na safari ya ughaibuni.

Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amesema ombi la awali la dola Milioni 72 kwaDjiboutikupitia mchakato wa Umoja wa Mataifa bado halijatekelezwa na sasa wanahitaji haraka fedha hizo kukwamua wahamiaji hao walio kwenye ofisi ya IOM huko Obok nchini humo.

Amesema miongoni mwao ni wanawake na watoto ambao walilaghaiwa kuwa watapata maisha mazuri lakini safari imekuwa ndefu ya uchovu, bila matumaini na hawana uwezo wowote wa kifedha. Jumbe amesema makundi  hayo yako hatarini kukumbwa na madhila ya ukatili kutoka wafanyabiashara haramu ya binadamu na amesihi jumuiya ya kimataifa kumulika hali hiyo kwani inazidi kuwa mbaya.