Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Kiethiopia na Kisomali wakwama Yemen IOM yaomba msaada

Wahamiaji wa Kiethiopia na Kisomali wakwama Yemen IOM yaomba msaada

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM nchini Djibouti  limetoa ombi la dharura la dola Milioni Tano kwa ajili ya kuokoa maisha ya wahamiaji wa Ethiopia na Somaliawalio kwenye mazingira magumu nchini humo baada ya kushindwa kuendelea na safari ya ughaibuni.

Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amesema ombi la awali la dola Milioni 72 kwa Djibouti kupitia mchakato wa Umoja wa Mataifa bado halijatekelezwa na sasa wanahitaji haraka fedha hizo kukwamua wahamiaji hao walio kwenye ofisi ya IOM huko Obok nchini humo.

Amesema miongoni mwao ni wanawake na watoto ambao walilaghaiwa kuwa watapata maisha mazuri lakini safari imekuwa ndefu ya uchovu, bila matumaini na hawana uwezo wowote wa kifedha. Amezungumza na Asumpta Massoi ungana nao