Madagascar inahitaji zaidi ya dola milioni 41 kupambana na janga la nzige

26 Machi 2013

Taifa la Madagascar linahitaji zaidi ya dola milioni 22 kwa ufadhili wa dharura hadi mwezi Juni kupambana na janga la nzige ambalo  linahatarisha usalama wa chakula kwa karibu nusu ya wananchi wa taifa hilo kwa mujibu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO. Shirikahilohata hivyo linasema kuwa mikakati ya miaka miwili inahitajika itakayogharimu kima cha dola milioni 19. Karibu nusu ya taifa ya taifa laMadagascarlimevamiwa na nzige suala linaloiweka kwenye hatari . Flora Nducha anaripoti.

(SAUTI YA FLORA NDUCHA)