Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi ya Ntaganda kuanza kusikilizwa Septemba 23 mwaka huu

Kesi ya Ntaganda kuanza kusikilizwa Septemba 23 mwaka huu

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imetangaza tarehe 23 mwezi Septemba kama siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili mtuhumiwa wa kivita nchini Jamhuri ya Kedomrasi ya Congo DRC Bosco Ntaganda.

Wakati wa kufikishwa mahakamani mara ya kwanza makaka ya ICC ilimtambua Ntaganda na kumfahamisha kuhusu mashataka yanayomkabili na haki zake chini ya makubaliano ya Roma.

(CLIP YA AFISA WA ICC)

“Kikao cha kwanza cha mahakama kilitangaza kuwa kuna ushahidi unaoonyesha kuwa bwana Ntaganda amehusika kwa uhalifu wa kivita ufuatao wa kivita.Uhalifu wa kuwaingiza watoto walio chini ya miaka mitano kwenye jeshi  wa kuwafanya kutenda uofu. Mauaji, ubakaji na uvamiuzi dhidi ya raia na utekaji nyara vyote vikiwa ni uhalifu wa kivita.”

Taarifa zaidi na George Njogopa

(RIPOTI YA GEORGE)