Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maonyesho ya mwaka 2015 kuhusu chakula kuandaliwa nchini Italia

Maonyesho ya mwaka 2015 kuhusu chakula kuandaliwa nchini Italia

Suala la kuhakikisha kuwepo kwa mifumo salama ya chakula litakuwa ajenda kuu kwenye maonyesho ya mwaka 2015 mjini Milan nchini Italia, kwa mujibu wa naibu Mkurugenzi mkuu wa kitengo cha misitu kwenye Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa  FAO Eduardo Rojas-Briales.

Kauli mbiu ya maonyesho hayo itakuwa “Kuilisha Sayari, Nguvu kwa Maisha”. Watakaoshiriki wataangazia masuala kama usalama wa chakula, wanawake, lishe , maendeleo ya kudumu na mabadiliko ya hali hewa.

Kwa mujibu wa Bwa. Rojas, changamoto  la  maonyesho ya mwaka 2015 ni kuchochea kuchukuliwa kwa hatua kama sehemu ya mikakati ya sasa ya kubuni mifumo ya chakula iliyo salama. Rojas amesema kuwa Umoja wa Mataifa utafanya kazi na washirika wake akiwemo mwandalizi wa maonyesho hayo Italia katika kubadilisha walichojifunza  katika jitihada za kuboresha maisha.

FAO kwa ushirikiano na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP  wataongoza maonyesho hayo kuambatana na ajenda zake.