Umoja wa Mataifa wawakumbuka waathiriwa wa utumwa

25 Machi 2013

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo linafanya hafla maalum ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa iliyofanyika kupitia Bahari ya Atlantiki. Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya kauli mbiu ‘Daima huru: kusherehekea ukombozi’, kama kumbukumbu ya ukombozi wa watumwa kote duniani.

Siku hii inaadhimishwa kwa heshima ya zaidi ya watu milioni 15 waliopitia machungu au kufa mikononi mwa mfumo uloendeleza unyama wa utumwa, ambao ulidumu takriban miaka 400. Siku hii pia inaadhimishwa ili kuchagiza ufahamu kuhusu hatari zitokanazo na ubaguzi wa rangi na aina nyingine za ubaguzi.

Maadhimisho ya leo ni ya miaka 150 tangu bunge la Marekani lilipopitisha azimio la kupiga marufuku utumwa, na yanatajumuisha hotuba kutoka kwa wasomi mashuhuri kama Profesa Ali