Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na ICC kushirikiana katika kesi dhidi ya Ntaganda: Ban

UM na ICC kushirikiana katika kesi dhidi ya Ntaganda: Ban

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imethibitisha kupelekwa The Hague kwa Bosco Ntaganda mtuhumiwa wa uhalifu wa  kibinadamu huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, hiyo ni hatua njema na ya kuungwa mkono. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika taarifa aliyotoa baada ya Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC kuthibitisha kuwa sasa Ntaganda yuko mikononi mwao. Bwana Ban amesema kitendo hicho kinaashiria kutokomezwa kwa tabia ya watuhumiwa wa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kwenye eneo hilo kukwepa sheria na amesisitiza tena kuwa kwa mujibu wa uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na ICC, Umoja wa Mataifa utatoa ushirikiano kuhakikisha Ntaganda anatendewa haki kwenye kesi hiyo na kwamba kesi hiyo inaendeshwa haraka.