Boda boda zaendelea kukatiza uhai wa watu kwenye ajali barabarani

22 Machi 2013

Ni hivi  karibuni tu shirika la afya duniani WHO lilitoa ripoti  inayoonesha kuwa ni mataifa 28 pekee yenye asilimia 7 ya watu wote duniani yana sheria madhubuti za usalama barabarani kwenye maeneo makuu matano ambayo ni kunywa pombe na kuendesha gari, mwendo kasi kupindukia, matumizi ya kofia kwa waendesha pikipiki, kufunga mikanda na matumizi ya viti maalum kwa watoto.

Katika ripoti hiyo Etenne Krug ambaye ni Mkurugenzi wa Kuzuia majanga  na ulemavu ndani ya WHO, amesema   hali ni mbaya zaidi barani Afrika ambapo ajali za pikipiki na baiskel ni kubwa na zinachangia vifo vingi vya ajali za barabarani.

Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha ya kwamba ajali nyingi za barabarani zinahusisha pikipiki kuliko magari. Takwimu za mwaka 2011 zinaonyesha ajali za pikipiki 5384 huku mwaka 2012 zikiongezeka hadi 5763.

Kufuatia hali hiyo Joseph Msami amefanya mahojaiano na kamanda wa kikosi cha usalama  barabarani chini Tanzania Muhamed  Mpinga ili kufahamau mikakati ya kikosi anachokiongoza katika kupambana na ongezeko la ajali za pikipiki.  Kamanda Mpinga anaeleza kikosi chake kinavyowafikia na kuwaelimisha madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda nchini Tanzania na kuanisha mikakati ya kuzuia ajali  kwa ujumla nchini humo.

SAUTI (KAMANDA MPINGA)