Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utamaduni wa kujenga amani Afrika kumulikwa: UNESCO

Utamaduni wa kujenga amani Afrika kumulikwa: UNESCO

Viongozi na watoa maamuzi barani Afrika, pamoja na wafanyabiashara mashuhuri, wachunguzi wa mambo na wasanii wanatazamia kuanza kukutana Luanda Angola kuanzia tarehe 26 hadi 28 Machi kwa ajili ya kujadili amani. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE)

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na serikali ya Angola linatazamiwa pia kuhudhuriwa na watu wengine mashuhuri. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova, Mwenyekiti wa Kamishna ya Umoja wa Afrika Nkosazana Diamini-Zuma na miongoni mwa viongozi wanaotazamia kuhudhuria ambao pia wanatazamia kutoa mhadhara. Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos,anatazamia kutoa hutuba ya ufunguzi, hotuba ambayo inaelezwa kuwa itaegemea mada ya amani na utulivu wa kisiasa. Walengwa wakubwa kwenye kongamano hilo ni  vijana wa umri wa kuanzia miaka 15 hadi 35 ambao ndiyo wanaochukua idadi kubwa barani afrika