Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuko tayari kusaidia uchunguzi wa ripoti za matumizi ya silaha za kemikali Syria: Pillay

Tuko tayari kusaidia uchunguzi wa ripoti za matumizi ya silaha za kemikali Syria: Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amekaribisha uamuzi wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon kufanya uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu madai kwamba huenda silaha za kemikali zimetumiwa nchini Syria.  Bi Pillay amesema ofisi ya haki za binadamu i tayari kusaidia katika uchunguzi huo.Hadi sasa hakuna ushahidi mkubwa unaoonyesha kwamba silaha za kemikali zimetumiwa. Hata hivyo, msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu, Rupert Colville, amesema ikigunduliwa kuwa kweli silaha za kemikali zimetumiwa, hicho kitakuwa kitendo kiovu mno na kosa la lisilokubaliwa kabisa.

(RUPERT COLVILLE 32”)

“Tunatumai ripoti hizi si sahihi, kwani ikiwa ni za kweli, basi mzozo huu utakuwa umezama na kufikia viwango vipya. Matumizi ya silaha za kemikali bila shaka utakuwa uhalifu wa dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivita. Kamishna Mkuu anaunga mkono ujumbe wa Katibu Mkuu kwamba kwamba ikiwa uhalifu kama huo umetendeka, wahusika ni lazima wawajibike kisheria. Wakati matokeo ya uchunguzi yakisubiriwa, Kamishna Mkuu anarudia mwito wake kwa pande zote katika mzozo kukomesha mara moja mashambulizi dhidi ya raia, na kuhakikisha usalama wao.”