UM wasaidia kuwanusuru watoto wakimbizi wa DRC wanaopotea

21 Machi 2013

Mapigano yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya vikosi vya waasi wa M23 na serikali ya nchi hiyo, yanaendelea kusababisha kadhia kwa raia ambapo kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia maswala ya misaada ya kibinadamu OCHA, idadi  ya wakimbizi wa ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni zaidi ya milioni moja na laki nane.

Idadi nyingine inayotajwa kuwa kubwa ni ya wakimbizi waliokimbilia nchi mbalimbali. Nchini Uganda pekee takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR zinaonyesha ya kwamba nchi hiyo inahifadhi wakimbizi elfu 81 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,miongoni mwao ni watoto.

Wengi wao hupotezana na wazazi na ndugu wengine wakati wa kutafuta hifadhi. Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake unafanya nini kuwanusuru watoto hawa? Ungana na Joseph Msami katika taarifa hii.